6 Juni 2021 - 12:12
Belfast yataka balozi wa Israel afukuzwe Ireland

Baraza la Mji Mkuu wa Ireland ya Kaskazini, Belfast limepasisha mpango wa kufukuzwa balozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel nchini humo na nchini Uingereza.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Sambamba na hatua hiyo ya Baraza la Mji wa Belfast ya kupasisha mpango wa kufukuzwa balozi wa Israel huko Ireland ya Kaskakzini, wanafunzi wa vyuo vikuu na wanaharakati watetezi wa haki za Palestina wamefanya maandamano na mgomo mbele ya jengo la Wizara ya Mambo ya Nje katika mji wa Dublin. 

Waandamanaji hao walikuwa wakipiga nara zinazoilaani serikali ya Israel na kutoa wito wa kufukuzwa balozi wa utawala huko katika mji wa Dublin.

Mpango wa kufukuzwa balozi wa Israel huko Ireland unasisitiza kuwa mashambulizi ya kikatili ya utawala huo wa Kizayuni dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza huko Palestina, mauaji ya kizazi na upanuzi wa ujenzi vitongoji haramu vya walowezi ni kinyume cha sheria za kimataifa.

Sehemu moja ya mpango huo inasema kuwa; Mashirika mengi ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu kama Human Rights Watch yanatambua hatua za Israel dhidi ya Wapalestina kuwa ni ubaguzi wa Apartheid. 

Uhalifu na mauaji yanayofanywa na Israel huko Palestina yanaendelea kupingwa na watetezi wa haki za binadamu katika nchi mbalimbali wanaofanya maandamano na makongamano ya kulaaji ukati na jinai hizo.  

342/